Kutambulisha Kitkit Shule

Kitikit ni shule inayotumia mfumo wa tabuleti yenye mtaala maalum wa kumuandaa mtoto kielimu pindi anapokua kwenye hatua za awali za kujifunza. Shule hii imejumuisha viwango vya kimataifa katika mazoezi ya akili na hesabu kwa mtindo na utaratibu unaokubalika ulimwenguni kote kujifunza ili kusaidia kila mtoto kufanikiwa kujifunza mwenyewe. Njia hii rahisi ya kujifunza inahuisha hali halisi ya maisha kwa kutumia katuni, michoro na picha zinazoakisi uhalisia ambao umebeba tamaduni mbalimbali na kuunganisha wanafunzi kutoka sehemu tofauti za ulimwengu kwa matokeo chanya.

 

kids in class and a tablet

Tulianzisha Kitkit Shule ili kuleta kiwango cha juu cha watoto kujifunza duniani kote. Kufanya hivyo, tulitumia tafiti yakinifu na uzoefu wetu wa miaka mingi kutengeneza elimu ya kipekee ya kidigitali,yenye viwango vya kimataifa kwa kuzingatia misingi ya ushirikishwaji, na kwa kutoa kipaumbele kwa mtoto kwa kutumia tabuleti. Kitkit Shule imeundwa kuwaandalia watoto msingi kwa mazoezi na kuwapatia ujuzi wa awali katika mazoezi ya akili na namba hata kama tayari watoto hao waliwahi kujiunga na shule, na inafanya hivyo kwa ushirikishwaji wa hali ya juu na mazingira yenye kuleta ufanisi ambayo hujitokeza mara tu wanapowasha tabuleti.

Mfumo wa kujifunza kwa Kitkit Shule unatoa elimu inayofaa kwani unampa mtoto fursa ya kusoma na kujifunza ujuzi muhimu unaohitajika kwenye mazoezi ya akili na hisabati kupitia vitabu, majaribio na kucheza michezo. Toleo hili la Kitkit Shule lina zaidi ya vitabu ishirini na tano (25) ambavyo ni sehemu ya mtaala wa upimaji akili, mazoezi ya kusoma  na michezo midogo midogo zaidi ya 200 kwa ajili ya hesabu na  mazoezi ya akili ya watoto wadogo.

Timu ya Todo Shule ni timu maalum ya Enuma Inc, ambayo ina lengo la kujenga teknolojia ya kipekee ya vifaa vya kujifunzia vitakavyosaidia kujenga uwezo na kujiamini kwa wanafunzi wanaopata tabu kujifunza ili wajifunze wenyewe. Ilianzishwa mwaka 2012 Berkeley, Carlofornia na mhandisi mwenye kiwango cha kimataifa pamoja na wazazi wabunifu wa michezo ya watoto ambao mtoto wao alizaliwa akiwa na mahitaji maalum. Kwa sasa, Enuma imekua na kuwa timu  ambayo imebuni michezo ya watoto kujifunza, hivyo kupelekea  kufanikiwa kibiashara, kutambulika zaidi na kupendwa na watumiaji wetu.