Timu ya Kitkit™ Shule ni timu maalum ya mradi ya Kampuni ya Enuma, Kampuni ambayo lengo lake ni kutengeneza zana za kiteknolojia ambazo zinatawasaidia wanafunzi walioko katika mazingira magumu kujifunza kupata kujiamini na kujifunza wenyewe huku wakijipatia ujuzi wa msingi. Ikiwa imeundwa mwaka 2012 Berkeley, California, na ikiwa na ofisi Seoul na Beijing.
Kampuni ya Enuma. Timu nyuma ya mradi wa Kitkit Shule imeunganisha miongo ya uzoefu wa pamoja kwenye elimu, michezo, uhandisi, muundo, na maendeleo ya kimataifa na kujitolea kwa pamoja kukuza elimu shirikishi na yenye usawa ambapo wanafunzi wote wanaweza wakafanikiwa.
Wafanyakazi wetu ambao ni waunda programu, wabunifu, na waelimishaji wanafanya kazi bila kuchoka na kwa lengo la kutengeneza ufumbuzi wa kujifunza kwa njia ya kidijitali ambao utashirikisha na kuwezesha.
Timu ya Kitkit Shule imechanganya ubora wake wa kiufundi pamoja na shauku yake ya kumaliza mahitaji yote ya kipekee ya watoto wote. Kwa kuingiza viwango bora vya kuunda michezo na tafiti kwenye elimu ya awali ya mtoto, sayansi ya neuro na nadharia ya kujifunza, Kitkit Shule imetengenezwa kuwezesha matokeo ya kujifunza yenye mafanikio kwa watoto wote, kuwafikia popote walipo na kuhimiza ushirikishwaji wa muda mrefu na hamasa ya kujifunza.
Timu yetu imejumuisha tafiti zinazoongoza kwenye sayansi ya neuro na elimu maalum, pamoja na mazoezi bora ya kimataifa kwenye kujifunza na mafunzo. Timu yetu pia inakusanya michakato kwa usalama, na kuunganisha taarifa za watumiaji kutoka kwenye programu zetu, ambazo tunazitumia kuimarisha matokeo ya kujifunza na matumizi.
Lengo la msingi la Enuma limekuwa watoto wenye uhitaji maalum au tofauti kwenye kujifunza, watoto ambao wanakosa rasilimali za kujifunzia na watoto ambao hawapati mifumo bora ya elimu.
Mafanikio ya programu zetu ambazo zinapatikana kibiashara — zikijumuisha Todo Math, Kid in story Book maker, na Visual Schedule for Children with autism — Imedhihirisha kujitolea kwetu kwenye kutengeneza bidhaa bora katika kuwawezesha watoto wote.
Ikiwa imeundwa mwaka 2012 na waunda michezo wawili ambao walihamasishwa na mtoto wao ambaye alikuwa ni mwenye uhitaji maalum, Enuma inaendeshwa na dhamira yake ya kuwashirikisha watoto na kuwawezesha wenye uhitaji maalum kujifunza wenyewe.
Sooinn Lee — Mkurugenzi mkuu
Gunho Lee — Mhandisi mkuu
“Kuunda Kitkit Shule, tumetumia miongo ya elimu, michezo, na uzoefu wa maendeleo ya kimataifa. Tunaamini watoto ambao hawawezi kupata shule, msaada na rasilimali au ambao wanapata shida shuleni wanahitaji zana bora za kujifunzia”
— Sooinn Lee, Mkurugenzi mkuu na Muongozaji wa ubunifu wa Enuma