Imeundwa kushirikisha na kuwezesha
Kitkit Shule imejumuisha mazoezi bora na tafiti zinazoongoza kwenye uundaji wa michezo pamoja na elimu ya kusoma, kuandika na kuhesabu kuwasaidia watoto kushiriki na kujifunza. Mfululizo wa kina wa kujifunza – Program yetu ya kujifunza yenye zaidi ya mazoezi 2,400, maktaba iliyoundwa ndani ikiwa na mamia ya vitabu na video, zana za kidijitali kwa ajili ya uchunguzi na kujieleza – kunawapa morali wanafunzi kujifunza kusoma, kuandika na kufanya hesabu za msingi ili kuweza kuwa wanafunzi wanaojitegemea na wenye hamasa ya kujifunza
Kwa wanafunzi tofauti
Timu yetu imetoa kipaumbele kwa wanafunzi tofauti, kama vile watoto wenye; uhitaji maalum, changamoto ya lugha, au wale ambao hawana hamasa ya kujifunza. Ikitumia mazoezi bora ya kimataifa kwenye kusoma, kuandika na hesabu ikiwa na muundo sawa wa kanuni za kujifunza, Kitkit Shule imeundwa kumsaidia kila mtoto kufanikiwa kama mwanafunzi huru
Matokeo yaliyooneshwa
Kama mshindi mwenza wa shindano la kujifunza la kidunia la XPRIZE, Kitkit Shule ilifikia matokeo ya juu katika washiriki wote watano waliofikia fainali katika shindano la katika shindano hili la kimataifa. Pia tumefanya majaribio kadhaa ambayo yalionyesha matokeo ya kujifunza yenye nguvu. (angalia chini kwa maelezo zaidi) Timu yetu inajivunia kuona Kitkit Shule ikitoa matokeo kwa makundi ambayo yametengwa, kwa kuwa inaonyesha dhamira yetu ya kuleta uzoefu wa kujifuza wenye ubora wa hali ya juu kwa wale wanaohitaji zaidi.