Ufumbuzi wa kina wa kujifunza
elimu ya awali kwa watoto WOTE

Tumetengeneza Kitkit shule ili kuleta uzoefu wa hali ya juu wa kujifunza kwa watoto wenye uhitaji zaidi duniani kote. Ikiwa imeitwa kwa neno “kufikiri” kwa Kithai, Kitkit Shule ni programu ambayo inapatikana kwenye tableti ikiwa na mtaala mpana ambao unaanzia kwenye hatua za awali za ukuaji wa mtoto hadi kwenye elimu ya awali. Imeundwa kumpa mtoto msingi na mazoezi yanayohitajika kujenga ujuzi wa msingi kwenye kusoma, kuandika na kuhesabu pamoja na fursa za kuchunguza masomo mengine yakiwepo muziki na sanaa–bila kujali upatikanaji wa shule au rasilimali.

Yaliyomo ndani

Kitkit Shule imeundwa kama jukwaa pana ambalo linajumuisha:

1. Programu ya kujifunzia iliyo katika mfumo wa michezo       2. Maktaba       3. Zana

1. Programu ya kujifunzia

Program ya kujifunzia ya Kitkit ni mfululizo wa mazoezi ya kielimu yanayoingiliana ambayo yanamfanya mtoto anajifunza na kufanya mazoezi yanayompa ujuzi wa msingi kwenye kusoma kuandika na hesabu. Toleo la sasa la Kitkit Shule linajumuisha kozi 22 za mayai ambazo zinajumuisha kusoma, kuandika na kuhesabu kwa awali ikiwa na shughuli za kujifunza takribani 2,400.

  • Inatoa msingi wa kidijitali wa kusoma na kuandika na ujuzi wa mapema unaohitajika kwa ajili ya baadae kwenye kujifunza kusoma, kuandika na hesabu
  • Uendelezaji uliowekwa wa ujuzi wa msingi wa kusoma na kuandika, kuanzia kwenye utambuzi wa herufi hadi utambuzi wa sauti na utambuzi wa maneno yaliyoandikwa
  • Kozi zinazoendelezwa zinaongeza ujuzi mpya na kuimarisha dhana ambazo zimeshapitiwa na kuleta ngazi nyingine ngumu zaidi
  • Maeneo ya msingi ya Kujifunza: Lugha ya mdomo / Utambuzi wa maneno yaliyoandikwa / kanuni za herufi / ufahamu wa sauti  / Sauti na herufi zilizoandikwa / Utamkaji wa herufi / Muundo wa maneno / Misamiati / Kusoma au kuandika kwa ufasaha / Maneno yaliyoandikwa / Ufahamu wa kusoma
  • Kozi 11 za Mayai / Takribani vipindi 280 / Takribani shughuli za kujifunza 1,200
  • Imetengenezwa kwenye uzoefu wa timu iliyotengeneza programu ya Todo Math, ambayo imeshinda tuzo, ambayo ni mfululizo mpana wa masomo kuanzia Kabla ya masomo ya awali hadi darasa la pili ikiwa imepakuliwa mara milioni 6 duniani kote
  • Inatumia uwakilishi wa picha nyingi na mbinu za kidijitali ambazo zinamsaidia mtoto kutengeneza ufahamu wa kina na uelewa wa dhana za kihesabu
  • Mtaala sawa wa hesabu ambao unajumuisha kuanzia kufuatisha namba hadi kuzidisha
  • Kozi 11 za mayai / Takribani vipindi 260 / Takribani shughuli za kujifunza 1,200

2. Maktaba

  • Vitabu katika ngazi mbalimbali: Kukiwa na zaidi ya vitabu 130 ambavyo vinafaa kiutamaduni kwenye ngazi saba tofauti kwa lengo la kutoa fursa “sahihi” za kujisomea
  • Kusoma kwa sauti: Kwa kubonyeza kitufe cha spika, watoto wanaweza wakasikia kitabu kikisomwa kwa sauti. Watoto wanaweza wakachagua neno moja moja kulisikia likisomwa kwa sauti, kuongeza ushiriki na uelewa
  • Mitindo mbalimbali na mada shirikishi: Inawaonyesha watoto aina mbali mbali za mitindo ikiwepo hadithi za uongo, hadithi za kweli, hadithi za watu mbalimbali na historia ya maisha ya watu. Inajumuisha mada mbalimbali shirikishi ikiwa ni pamoja na wanyama, sayansi, urafiki, na watu wa kuigwa
  • Maudhui sahihi kiutamaduni: imetengenezwa kuwa sahihi kiutamaduni kwa watoto katika nchi zinazoendelea. Inajumuisha usawa wa washiriki wa kiume na wa kike ili kukuza utofauti chanya wa mifano ya kijinsia. Imetengenezwa na Enuma kwa kushirikiana na Ubongo Kids, Kampuni ya chombo cha habari kwa ajili ya watoto iliyoko Tanzania

3. Zana

  • Zinasaidia watoto kujenga uwezo wa kidijitali na kuwapatia fursa muhimu ya kujieleza wenyewe kwa kupitia sanaa na muziki
  • Watoto wanachagua kati ya zana 8 za kujifunzia ambazo zinawapa kujiamini kwenye mawazo na uwezo wao
  • Inajumuisha vyombo ambavyo sio halisi, ubao wa kufanyia mazoezi ya kuandika, na zana za kuchorea na kupakia rangi ili kutengeneza kazi za kipekee za sanaa
  • Majaribio yetu mpaka sasa yameonyesha ushiriki mkubwa wa watoto kwa kutumia hizi zana ambazo zinawaruhusu kuonyesha ubunifu wao

Kwa nini Kitkit Shule

Ujuzi wa Msingi

Kujifunza kumetengenezwa kuwezesha maendeleo ya utambuzi na uchunguzi binafsi kadri mwanafunzi anavyojifunza kusoma, kuandika na hesabu

Kujifunza binafsi

Imemlenga hasa mtoto, muonekano wake ambao unamvutia mtoto unahakikisha kuwa kila mtoto anakuwa na uwezo wa kufanikiwa

Upatikanaji

Picha zenye muonekano wa asili na sifa za upatikanaji zinajumuisha na kuwawezesha wanafunzi tofauti tofauti wanaojifunza ulimwenguni

Jifunze zaidi kuhusu falsafa ya Kujifunza ya Kitkit Shule, namna ya uundwaji wake na mfumo wa mtaala

Kitkit Shule imeunganisha mazoezi bora ya kimataifa kwenye kusoma, kuandika na elimu ya hesabu ikiwa na muundo sawa wa kanuni za kujifunza kumsaidia kila mtoto aweze kufanikiwa kama mwanafunzi huru. Muundo unaoweza kubadilika wa Kitkit Shule unakuja na uzoefu unaovutia na shirikishi ambao unaondoa tofauti za kitamaduni na kutengeneza matokeo chanya ya kielimu kwa wanafunzi tofauti tofauti ulimwenguni. Unaweza ukajifunza zaidi kuhusu falsafa yetu ya kujifunza, muundo, na utafiti uliotumika kutengeneza Kitkit Shule kwa kupakua hati yetu ya Kujifunza na kuunda ya Kitkit Shule hapa.

Vifaa vyenye uwezo

Sifa za chini za Tableti

  • Toleo la OS: Kuanzia Android 6.0 hadi 9.0
  • RAM: Kuanzia 1.7 GB ila inayopendekezwa ni 2.0 GB
  • Uwezo wa ndani: Kuanzia 16GB ikiwa na 6GB ambazo ziko wazi
  • Ukubwa wa kioo 1280 x 800