Athari Yetu

Matokeo yenye nguvu, ATHARI inayoonekana

Kitkit Shule inabadili kujifunza na kutoa matokeo yenye nguvu kwa watoto, bila kujali uwezo wao wa awali na upatikanaji wa rasilimali. Tangu Kitkit iundwe mwaka 2016, mashirika tunayoshirikiana nayo yamewezesha athari yetu inayokua, kuifikisha Kitkit Shule kwa watoto na pia kwa watoto walio katika jamii ngumu kufikika duniani kote.

Programu yetu pana ya kujifunzia imeonyesha…

  • Ongezeka kwenye kusoma, kuandika na kuhesabu
  • Matokeo yaliyoboreka kwa wale wanaoyahitaji zaidi
  • Faida za kimabadiliko hata zaidi ya elimu

Shindano la Kujifunza la Kidunia la XPRIZE

Kitkit Shule inajivunia kuwa mshindi mwenza wa Dola za Kimarekani Milioni 15 za Shindano la Kujifunza la Kidunia la XPRIZE ambalo linazitaka timu mbalimbali kutoka ulimwenguni kote kutengeneza programu za wazi ambazo zinaweza kupanuliwa ili kuweza kuwasaidia watoto kujifunza wenyewe kusoma, kuandika na kuhesabu.

XPRIZE, ikiwa inashirikiana na UNESCO, Shirika la chakula duniani, na Wizara ya Elimu Tanzania, ilifanya majaribio kwenye vijiji yaliyochukua miezi 15 yakijumuisha watoto 3,000 kutoka Tanzania kwa kutumia ufumbuzi kutoka kwa washindi watano. Takribani watoto 450 kwenye vijiji 30 walitumia Kitkit Shule. Wakati washindi wote watano walionyesha matokeo mazuri kwenye kujifunza lakini tuzo ilitolewa kwa waliofanya vizuri zaidi.

Cox's Bazar, BANGLADESH

Kwa kushirikiana na Kamati ya uokoaji ya kimataifa na Fikiria Ulimwenguni(Imagine Worldwide), tunaileta Kitkit Shule kwa ajili ya wanafunzi wa Rohingya katika eneo la Cox’s Bazar, Bangladesh. Hadi sasa, zaidi wa Warohingya 900,000 wamekimbia vurugu na mateso nchini Myanmar kutafuta hifadhi eneo la Cox’s Bazar, na zaidi ya nusu ya waliohamishwa ni Watoto au vijana wadogo. Kama inavyokadiriwa kuwa wengi wa watoto wa Rohingya wanaripotiwa kuwa hawajawahi kushiriki katika mfumo wowote wa masomo kabla na baada ya kuja Bangladesh, uhitaji wa elimu bora ni wa haraka sana.

Ni heshima kwetu kuwaletea utatuzi wetu wa kiteknolojia uliotengenezwa kwa ajili ya mazingira husika kwa kupitia majumbani na kwenye vituo vya kujifunzia na pia kwenye kambi, pamoja na washirika wetu waliojitolea, kama sehemu ya mwitikio wa mapema kwenye dharura hii.

Mtwara and Bagamoyo, TANZANIA

Mwaka 2017 Utafiti uliodhibitiwa ulionyesha kuwa Kitkit iliweza kufanya vizuri kwenye kuboresha matokeo ya kujifunza kwa wote waliopo shuleni na wale ambao hawapo katika mazingira ya shuleni, kujenga ujuzi wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa wanafunzi 100 kwa zaidi ya miezi mitatu kwa makundi mawili ya majaribio: 1) Wenye umri wa miaka 6 mpaka 10 kwenye kituo cha jamii, 2) Kundi lililotumia Kitkit la wanafunzi wa darasa la 1 hadi la 3 kwenye shule ya msingi kijijini.

Matokeo yanatia moyo sana, sanasana kwa muktadha wa Tanzania ambapo asilimia 23.2 ya watoto kati ya miaka 7 hadi 14 hawajaandikishwa shuleni kutokana na sababu mbalimbali. Matokeo yetu yalionyesha kwamba mbinu inayohamishika ya kiteknolojia ikitumika kama zana ya kielimu ina uwezo mkubwa sana kuwezesha “Kujiongoza Mwenyewe” Katika kujifunza kwa watoto kwenye maeneo ya vijijini

Kambi ya wakimbizi ya Kakuma, KENYA

Mradi wa Xavier ulishirikiana na Enuma kuboresha upatikanaji wa Elimu kwa wakimbizi 240 na watoto wa jamii wenyeji wao kwa kutumia Kitkit Shule katika Shule ya Msingi Kolobeyei katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma.

Kwa kundi la wanafunzi 35 waliochaguliwa bila mpangilio maalum na kuchunguzwa, Matokeo yalikuwa makubwa… sana sana kwa wale ambao walihitaji msaada zaidi. Kwa dakika 30 za kujifunza wenyewe kila siku kwa kutumia Kitkit Shule kwa wiki 8, wanafunzi kwenye makazi ya Kalobeyei waliongeza matokeo yao baada ya jaribio kwa wastani wa tarakimu mbili kwenye kusoma na kuandika na hesabu.

Shule ya Msingi Kagina, RWANDA

Shirika la Majirani Wema(Good Neighbours) Rwanda walishirikiana na Kampuni ya Enuma kuwawezesha wanafunzi katika shule ya msingi Kagina, Rwanda kwa ujuzi wa elimu ya Kingereza, kusoma kuandika na hesabu kwa ajili ya kuwaandaa kwa kuanza kutumia lugha ya Kiingereza kama lugha ya Kiofisi badala ya Lugha ya Kinyarwanda kwa darasa la 4. Kutoka mwezi wa tisa hadi wa kumi na mbili mwaka 2018, wanafunzi 684 walishiriki kwenye fursa wa wiki 25.

Wanafunzi walionyesha matokeo makubwa kwenye kujifunza na uwiano chanya wa muda uliotumika kufikia mafanikio makubwa

MUHTASARI WA ATHARI

“Toka hapo Nashim amekuwa mwanachama hai wa darasa la Kitkit…. Kitkit Shule imemhamasisha kuja shuleni kila siku”
“Nilishangazwa. Watoto wameonyesha kuwa wana uwezo wa kiasili wa kuchunguza wenyewe”
“Mradi huu umenihamasisha mimi na wanafunzi darasani kwangu. Nimeona mabadiliko mengi kwa wanafunzi wangu kama sasa hivi wanaweza wakasoma na kuandika na wanaweza pia wakafanya hesabu vizuri”
“Mradi wa Kitkit umeleta maboresho makubwa shuleni kwetu, Mojawapo wa wasichana kutoka darasa la kitkit amepiga hatua kubwa hadi kufikia nafasi ya tatu kwa muhula huu”
“Mpango umewasaidia wanafunzi sana kuboreka. Kama mwalimu, nimejikuta napata urahisi kufundisha darasani kwa sababu wanafunzi walikuwa wamehamasika na wanashiriki kikamilifu”
“Mara tu wanafunzi wakishaingia wanaanza kujifunza, na sijawahi kuona wanafunzi 30 darasani wakiwa wanajifunza kwa makini vile”
“Tulivyoanzisha darasa la Kitkit, Kulikuwa na watoro wengi sana. Ila kadri tulivyoendelea, watoto wengi sana walijisikia kuhamasika kuendelea kuja shuleni kila siku”
“Toka hapo Nashim amekuwa mwanachama hai wa darasa la Kitkit…. Kitkit Shule imemhamasisha kuja shuleni kila siku”
“Nilishangazwa. Watoto wameonyesha kuwa wana uwezo wa kiasili wa kuchunguza wenyewe”
“Mradi huu umenihamasisha mimi na wanafunzi darasani kwangu. Nimeona mabadiliko mengi kwa wanafunzi wangu kama sasa hivi wanaweza wakasoma na kuandika na wanaweza pia wakafanya hesabu vizuri”
“Mradi wa Kitkit umeleta maboresho makubwa shuleni kwetu, Mojawapo wa wasichana kutoka darasa la kitkit amepiga hatua kubwa hadi kufikia nafasi ya tatu kwa muhula huu”